وَقَالَ يَٰبَنِىَّ لَا تَدْخُلُوا۟ مِنۢ بَابٍ وَٰحِدٍ وَٱدْخُلُوا۟ مِنْ أَبْوَٰبٍ مُّتَفَرِّقَةٍ وَمَآ أُغْنِى عَنكُم مِّنَ ٱللَّهِ مِن شَىْءٍ إِنِ ٱلْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَعَلَيْهِ فَلْيَتَوَكَّلِ ٱلْمُتَوَكِّلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa akasema: Enyi wanangu! Msiingie kupitia mlango mmoja, bali ingieni kwa kupitia milango tofautitofauti. Wala mimi siwafai kitu mbele ya Mwenyezi Mungu. Hukumu haiko isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu tu. Juu yake mimi nimetegemea, na juu yake na wategemee wanaotegemea.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa akasema: Enyi wanangu! Msiingie mlango mmoja, bali ingieni kwa milango mbali mbali. Wala mimi sikufaeni kitu mbele ya Mwenyezi Mungu. Hukumu haiko ila kwa Mwenyezi Mungu tu. Juu yake Yeye mimi nimetegemea, na juu yake Yeye wategemee wanao tegemea.