وَمَا ظَلَمْنَٰهُمْ وَلَٰكِن ظَلَمُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ فَمَآ أَغْنَتْ عَنْهُمْ ءَالِهَتُهُمُ ٱلَّتِى يَدْعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مِن شَىْءٍ لَّمَّا جَآءَ أَمْرُ رَبِّكَ وَمَا زَادُوهُمْ غَيْرَ تَتْبِيبٍ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Sisi hatukuwadhulumu, lakini wao wenyewe walizidhulumu nafsi zao. Na miungu yao waliyokuwa wakiiomba badala ya Mwenyezi Mungu haikuwafaa kitu ilipokuja amri ya Mola wako Mlezi. Na hiyo miungu haikuwazidishia isipokuwa maangamio tu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa Sisi hatukuwadhulumu, lakini wao wenyewe wamejidhulumu. Na miungu yao waliyo kuwa wakiiomba badala ya Mwenyezi Mungu haikuwafaa kitu ilipo kuja amri ya Mola wako Mlezi. Na hiyo miungu haikuwazidishia ila maangamizo tu.