تَرَىٰ كَثِيرًا مِّنْهُمْ يَتَوَلَّوْنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَبِئْسَ مَا قَدَّمَتْ لَهُمْ أَنفُسُهُمْ أَن سَخِطَ ٱللَّهُ عَلَيْهِمْ وَفِى ٱلْعَذَابِ هُمْ خَٰلِدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterUtawaona wengi miongoni mwao wanafanya urafiki wandani na wale waliokufuru. Hakika ni maovu mno ziliyozitanguliza nafsi zao hata Mwenyezi Mungu akawakasirikia, nao watadumu katika adhabu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniUtawaona wengi wao wanafanya urafiki na walio kufuru. Hakika ni maovu yaliyo tangulizwa na nafsi zao hata Mwenyezi Mungu amewakasirikia, nao watadumu katika adhabu.