caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Maaida, Aya 60

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 112 · 5:60

قُلْ هَلْ أُنَبِّئُكُم بِشَرٍّ مِّن ذَٰلِكَ مَثُوبَةً عِندَ ٱللَّهِ مَن لَّعَنَهُ ٱللَّهُ وَغَضِبَ عَلَيْهِ وَجَعَلَ مِنْهُمُ ٱلْقِرَدَةَ وَٱلْخَنَازِيرَ وَعَبَدَ ٱلطَّٰغُوتَ أُو۟لَٰٓئِكَ شَرٌّ مَّكَانًا وَأَضَلُّ عَن سَوَآءِ ٱلسَّبِيلِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Je, niwaambie lililo baya zaidi kuliko hilo katika malipo mbele ya Mwenyezi Mungu? Ni yule ambaye Mwenyezi Mungu alimlaani na akamkasirikia, na akawafanya miongoni mwao manyani na nguruwe, na wakamuabudu Shetani. Hao ndio wenye mahali pabaya zaidi na waliopotea zaidi njia iliyo sawa.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniSema: Je! Nikwambieni yule ambaye ni mwenye malipo mabaya zaidi kuliko hayo mbele ya Mwenyezi Mungu? Ni yule ambaye Mwenyezi Mungu amemlaani na amemkasirikia, na amewafanya miongoni mwao manyani na nguruwe, na wakamuabudu Shet'ani. Hao ndio wenye mahali pabaya na wamepotea zaidi njia iliyo sawa.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70