بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَوْفُوا۟ بِٱلْعُقُودِ أُحِلَّتْ لَكُم بَهِيمَةُ ٱلْأَنْعَٰمِ إِلَّا مَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ غَيْرَ مُحِلِّى ٱلصَّيْدِ وَأَنتُمْ حُرُمٌ إِنَّ ٱللَّهَ يَحْكُمُ مَا يُرِيدُ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Timizeni mapatano. Mmehalalishiwa wanyama wa kufugwa, isipokuwa wale mnaosomewa. Lakini msihalalishe kuwinda hali ya kuwa mko katika Ihram. Hakika, Mwenyezi Mungu anahukumu apendavyo.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniEnyi mlio amini! Timizeni ahadi. Mmehalalishiwa wanyama wa mifugo, ila wale mnao tajiwa. Lakini msihalalishe kuwinda nanyi mmo katika Hija. Hakika Mwenyezi Mungu anahukumu apendavyo.