caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura An-Nisaa, Aya 83

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 92 · 4:83

وَإِذَا جَآءَهُمْ أَمْرٌ مِّنَ ٱلْأَمْنِ أَوِ ٱلْخَوْفِ أَذَاعُوا۟ بِهِۦ وَلَوْ رَدُّوهُ إِلَى ٱلرَّسُولِ وَإِلَىٰٓ أُو۟لِى ٱلْأَمْرِ مِنْهُمْ لَعَلِمَهُ ٱلَّذِينَ يَسْتَنۢبِطُونَهُۥ مِنْهُمْ وَلَوْلَا فَضْلُ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُۥ لَٱتَّبَعْتُمُ ٱلشَّيْطَٰنَ إِلَّا قَلِيلًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa linapowajia jambo lolote linalohusiana na amani au hofu, wao wanalitangaza. Na lau kuwa wangelipeleka hilo kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanaochunguza miongoni mwao wangelijua. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake, mngelimfuata Shetani isipokuwa wachache tu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa linapo wafikia jambo lolote lilio khusu amani au la kitisho wao hulitangaza. Na lau kuwa wangeli lipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanao chunguza wangeli lijua. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake mngeli mfuata Shet'ani ila wachache wenu tu.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70