وَلَوْ أَنَّا كَتَبْنَا عَلَيْهِمْ أَنِ ٱقْتُلُوٓا۟ أَنفُسَكُمْ أَوِ ٱخْرُجُوا۟ مِن دِيَٰرِكُم مَّا فَعَلُوهُ إِلَّا قَلِيلٌ مِّنْهُمْ وَلَوْ أَنَّهُمْ فَعَلُوا۟ مَا يُوعَظُونَ بِهِۦ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ وَأَشَدَّ تَثْبِيتًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau kuwa tuliwaandikia kuwa: 'Jiueni, au tokeni majumbani mwenu', wasingeliyafanya hayo isipokuwa wachache tu miongoni mwao. Na lau kama wangeliyafanya yale wanayowaidhiwa kwayo, ingelikuwa bora kwao na uthibitisho wa nguvu zaidi.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa lau kuwa tumewaamrisha: Jiueni, au tokeni majumbani kwenu, wasingeli fanya hayo ila wachache tu miongoni mwao. Na lau kama wangeli fanya walio waidhiwa ingeli kuwa bora kwao na uthibitisho wa nguvu zaidi.