أُو۟لَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ يَعْلَمُ ٱللَّهُ مَا فِى قُلُوبِهِمْ فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَعِظْهُمْ وَقُل لَّهُمْ فِىٓ أَنفُسِهِمْ قَوْلًۢا بَلِيغًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu anayajua yaliyo katika nyoyo zao. Basi wapuuze, na uwawaidhi, na uwaambie maneno ya kuathiri na kuingia katika nafsi zao.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniHao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo ndani ya nyoyo zao. Basi waachilie mbali, uwape mawaidha na uwaambie maneno ya kuathiri na kuingia katika nafsi zao.