فَمِنْهُم مَّنْ ءَامَنَ بِهِۦ وَمِنْهُم مَّن صَدَّ عَنْهُ وَكَفَىٰ بِجَهَنَّمَ سَعِيرًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi miongoni mwao kuna yule aliyemwamini, na miongoni mwao kuna yule aliyemkufuru. Na Jahannamu inatosha kuwa ndio moto wenye mwako mkali.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniBasi wapo miongoni mwao waliyo yaamini, na wapo walio yakataa. Na Jahannamu yatosha kuwa ni moto wa kuwateketeza.