caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Faatir, Aya 45

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 43 · 35:45

وَلَوْ يُؤَاخِذُ ٱللَّهُ ٱلنَّاسَ بِمَا كَسَبُوا۟ مَا تَرَكَ عَلَىٰ ظَهْرِهَا مِن دَآبَّةٍ وَلَٰكِن يُؤَخِّرُهُمْ إِلَىٰٓ أَجَلٍ مُّسَمًّى فَإِذَا جَآءَ أَجَلُهُمْ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِعِبَادِهِۦ بَصِيرًۢا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau kuwa Mwenyezi Mungu angeliwachukulia watu kwa yale waliyoyachuma, basi asingelimuacha juu ya ardhi hata mnyama mmoja. Lakini Yeye anawaachilia mpaka ufike muda maalumu. Na muda wao ukifika, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja wake barabara.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli wachukulia watu kwa waliyo yachuma, basi asingeli muacha juu ya ardhi hata mnyama mmoja. Lakini Yeye anawachukulia mpaka ufike muda maalumu. Basi ukifika muda wao basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja wake baraabara.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70