caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Faatir, Aya 11

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 43 · 35:11

وَٱللَّهُ خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ جَعَلَكُمْ أَزْوَٰجًا وَمَا تَحْمِلُ مِنْ أُنثَىٰ وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلْمِهِۦ وَمَا يُعَمَّرُ مِن مُّعَمَّرٍ وَلَا يُنقَصُ مِنْ عُمُرِهِۦٓ إِلَّا فِى كِتَٰبٍ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu amewaumba kutokana na udongo. Kisha kwa tone la manii. Kisha akawafanya mwanamume na mwanamke. Na mwanamke yeyote hachukui mimba, wala hazai, isipokuwa kwa elimu yake. Na wala hapewi umri mwenye umri mrefu, wala hapunguziwi katika umri wake, isipokuwa yamo hayo katika Kitabu. Hakika hayo ni mepesi kwa Mwenyezi Mungu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa Mwenyezi Mungu amekuumbeni kutokana na udongo. Kisha kwa tone la manii. Kisha akakufanyeni mwanamume na mwanamke. Na mwanamke yeyote hachukui mimba, wala hazai, ila kwa ilimu yake. Na wala hapewi umri mwenye umri mrefu, wala hapunguziwi katika umri wake, ila yamo hayo katika Kitabu. Hakika hayo ni mepesi kwa Mwenyezi Mungu.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70