caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Ahzaab, Aya 35

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 90 · 33:35

إِنَّ ٱلْمُسْلِمِينَ وَٱلْمُسْلِمَٰتِ وَٱلْمُؤْمِنِينَ وَٱلْمُؤْمِنَٰتِ وَٱلْقَٰنِتِينَ وَٱلْقَٰنِتَٰتِ وَٱلصَّٰدِقِينَ وَٱلصَّٰدِقَٰتِ وَٱلصَّٰبِرِينَ وَٱلصَّٰبِرَٰتِ وَٱلْخَٰشِعِينَ وَٱلْخَٰشِعَٰتِ وَٱلْمُتَصَدِّقِينَ وَٱلْمُتَصَدِّقَٰتِ وَٱلصَّٰٓئِمِينَ وَٱلصَّٰٓئِمَٰتِ وَٱلْحَٰفِظِينَ فُرُوجَهُمْ وَٱلْحَٰفِظَٰتِ وَٱلذَّٰكِرِينَ ٱللَّهَ كَثِيرًا وَٱلذَّٰكِرَٰتِ أَعَدَّ ٱللَّهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na wanaume watiifu na wanawake watiifu, na wanaume wakweli na wanawake wakweli, na wanaume wanaosubiri, na wanawake wanaosubiri, na wanaume wanyenyekevu na wanawake wanyenyekevu, na wanaume watoao sadaka na wanawake watoao sadaka, na wanaume wanaofunga saumu na wanawake wanaofunga saumu, na wanaume wanaojihifadhi tupu zao, na wanawake wanaojihifadhi tupu zao, na wanaume wanaomdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi na wanawake wanaomdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi, Mwenyezi Mungu amewaandalia msamaha na ujira mkubwa.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniHakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na wat'iifu wanaume na wat'iifu wanawake, na wasemao kweli wanaume na wanawake, na wanao subiri wanaume na wanawake, na wanyenyekevu wanaume na wanawake, na watoao sadaka wanaume na wanawake, na wanao funga wanaume na wanawake, na wanao jihifadhi tupu zao wanaume na wanawake, na wanao mdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi wanaume na wanawake, Mwenyezi Mungu amewaandalia msamaha na ujira mkubwa.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70