يَحْسَبُونَ ٱلْأَحْزَابَ لَمْ يَذْهَبُوا۟ وَإِن يَأْتِ ٱلْأَحْزَابُ يَوَدُّوا۟ لَوْ أَنَّهُم بَادُونَ فِى ٱلْأَعْرَابِ يَسْـَٔلُونَ عَنْ أَنۢبَآئِكُمْ وَلَوْ كَانُوا۟ فِيكُم مَّا قَٰتَلُوٓا۟ إِلَّا قَلِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanafikiri yale makundi ya maadui hayajaondoka. Na yakija hayo makundi, watatamani laiti wao wako majangwani pamoja na mabedui, wakiuliza habari zenu. Na lau wangekuwa pamoja nanyi, basi hawangepigana isipokuwa kidogo tu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWanafikiri yale makundi ya maadui hayajaondoka. Na yakija hayo makundi watatamani laiti wao wako majangwani pamoja na mabedui, wakiuliza khabari zenu. Na lau wakiwa pamoja nanyi hawapigani ila kidogo tu.