ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ فِى ٱلسَّرَّآءِ وَٱلضَّرَّآءِ وَٱلْكَٰظِمِينَ ٱلْغَيْظَ وَٱلْعَافِينَ عَنِ ٱلنَّاسِ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلْمُحْسِنِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale ambao hutoa wanapokuwa katika nyakati nzuri na wanapokuwa katika dhiki, na wanajizuia ghadhabu, na ni wasamehevu kwa watu. Na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniAmbao hutoa wanapo kuwa na wasaa na wanapo kuwa na dhiki, na wanajizuia ghadhabu, na wasamehevu kwa watu; na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema;