وَلَا يَأْتَلِ أُو۟لُوا۟ ٱلْفَضْلِ مِنكُمْ وَٱلسَّعَةِ أَن يُؤْتُوٓا۟ أُو۟لِى ٱلْقُرْبَىٰ وَٱلْمَسَٰكِينَ وَٱلْمُهَٰجِرِينَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلْيَعْفُوا۟ وَلْيَصْفَحُوٓا۟ أَلَا تُحِبُّونَ أَن يَغْفِرَ ٱللَّهُ لَكُمْ وَٱللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale katika nyinyi wenye fadhila na wasaa wasiape kutowapa jamaa zao, na masikini na waliohama kwa Njia ya Mwenyezi Mungu. Na wasamehe, na waachilie mbali. Je, nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu awasamehe? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa wale katika nyinyi wenye fadhila na wasaa wasiape kutowapa jamaa zao na masikini na walio hama kwa Njia ya Mwenyezi Mungu. Na wasamehe, na waachilie mbali. Je! Nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu akusameheni? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.