caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Baqara, Aya 256

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 87 · 2:256

لَآ إِكْرَاهَ فِى ٱلدِّينِ قَد تَّبَيَّنَ ٱلرُّشْدُ مِنَ ٱلْغَىِّ فَمَن يَكْفُرْ بِٱلطَّٰغُوتِ وَيُؤْمِنۢ بِٱللَّهِ فَقَدِ ٱسْتَمْسَكَ بِٱلْعُرْوَةِ ٱلْوُثْقَىٰ لَا ٱنفِصَامَ لَهَا وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakuna kulazimisha katika Dini. Kwani uongofu umekwishapambanuka kutokana na upotovu. Kwa hivyo, anayemkufuru Taaghuut na akamwamini Mwenyezi Mungu, basi bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisichovunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia mno, Mwenye kujua vyema.[1]
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniHapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet'ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70