لَّا يُؤَاخِذُكُمُ ٱللَّهُ بِٱللَّغْوِ فِىٓ أَيْمَٰنِكُمْ وَلَٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا كَسَبَتْ قُلُوبُكُمْ وَٱللَّهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu hawachukulii ubaya katika viapo vyenu ambavyo hamkuvikusudia. Lakini anawachukulia ubaya kwa yale ambayo nyoyo zenu zinachuma. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mpole.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniMwenyezi Mungu hakushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi. Bali anakushikeni kwa yanayo chuma nyoyo zenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mpole.