caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Baqara, Aya 105

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 87 · 2:105

مَّا يَوَدُّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِنْ أَهْلِ ٱلْكِتَٰبِ وَلَا ٱلْمُشْرِكِينَ أَن يُنَزَّلَ عَلَيْكُم مِّنْ خَيْرٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَٱللَّهُ يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِۦ مَن يَشَآءُ وَٱللَّهُ ذُو ٱلْفَضْلِ ٱلْعَظِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWaliokufuru miongoni mwa watu wa Kitabu na washirikina hawapendi mteremshiwe heri yoyote kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na Mwenyezi Mungu humteuwa amtakaye kumpa rehema yake. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila kubwa.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWalio kufuru miongoni mwa watu wa Kitabu na washirikina hawapendi mteremshiwe kheri yoyote kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na Mwenyezi Mungu humkusudia kumpa rehema yake ampendaye. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila kubwa.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70