وَرَٰوَدَتْهُ ٱلَّتِى هُوَ فِى بَيْتِهَا عَن نَّفْسِهِۦ وَغَلَّقَتِ ٱلْأَبْوَٰبَ وَقَالَتْ هَيْتَ لَكَ قَالَ مَعَاذَ ٱللَّهِ إِنَّهُۥ رَبِّىٓ أَحْسَنَ مَثْوَاىَ إِنَّهُۥ لَا يُفْلِحُ ٱلظَّٰلِمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa yule bibi wa nyumba aliyokuwamo Yusuf akamtamani kinyume cha nafsi yake, na akafungafunga milango. Akamwambia: "Njoo!" Yusuf akasema: Audhubillahi (ninajikinga kwa Mwenyezi Mungu)! Hakika Yeye ni bwana wangu, aliniweka maskani nzuri. Hakika madhalimu hawafaulu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa yule bibi wa nyumba aliyo kuwamo Yusuf alimtamani kinyume cha nafsi yake, na akafunga milango. Akamwambia: Njoo! Yusuf akasema: Audhubillahi! Najikinga na Mwenyezi Mungu. Huyu bwana wangu kaniweka maskani nzuri, na hakika wenye kudhulumu hawatengenekewi.