بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ الٓر كِتَٰبٌ أُحْكِمَتْ ءَايَٰتُهُۥ ثُمَّ فُصِّلَتْ مِن لَّدُنْ حَكِيمٍ خَبِيرٍ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAlif Laam Raa.[1] Hiki ni Kitabu ambacho Aya zake zimefanywa kuwa sawasawa, kisha zikapambanuliwa kwa kina, kilichotoka kwa Mwenye Hekima, Mwenye habari zote.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniAlif Lam Ra. Hiki ni Kitabu ambacho Aya zake zimewekwa wazi, kisha zikapambanuliwa, kilicho toka kwa Mwenye Hikima na Mwenye Khabari!