هُوَ ٱلَّذِى بَعَثَ فِى ٱلْأُمِّيِّـۧنَ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُوا۟ عَلَيْهِمْ ءَايَٰتِهِۦ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ ٱلْكِتَٰبَ وَٱلْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا۟ مِن قَبْلُ لَفِى ضَلَٰلٍ مُّبِينٍ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye ndiye aliyemtuma Mtume kwenye watu wasiojua kusoma na kuandika, awasomee Aya zake na awatakase, na awafunze Kitabu na hekima, ijapokuwa kabla ya haya walikuwa katika upotovu ulio dhahiri.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniYeye ndiye aliye mpeleka Mtume kwenye watu wasio jua kusoma, awasomee Aya zake na awatakase, na awafunze Kitabu na hikima, ijapo kuwa kabla ya haya walikuwa katika upotofu ulio dhaahiri.