caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Maaida, Aya 72

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 112 · 5:72

لَقَدْ كَفَرَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓا۟ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْمَسِيحُ ٱبْنُ مَرْيَمَ وَقَالَ ٱلْمَسِيحُ يَٰبَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ رَبِّى وَرَبَّكُمْ إِنَّهُۥ مَن يُشْرِكْ بِٱللَّهِ فَقَدْ حَرَّمَ ٱللَّهُ عَلَيْهِ ٱلْجَنَّةَ وَمَأْوَىٰهُ ٱلنَّارُ وَمَا لِلظَّٰلِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika, wamekufuru wale waliosema: 'Hakika, Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryam!' Na hali Masihi mwenyewe alisema: 'Enyi Wana wa Israili! Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Kwani, mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu amemharamishia Bustani ya mbinguni, na pahali pake ni Motoni. Na madhalimu hawatakuwa na wowote wa kuwanusuru.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniHakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryamu! Na hali Masihi mwenyewe alisema: Enyi Wana wa Israili! Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70