caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Maaida, Aya 7

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 112 · 5:7

وَٱذْكُرُوا۟ نِعْمَةَ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ وَمِيثَٰقَهُ ٱلَّذِى وَاثَقَكُم بِهِۦٓ إِذْ قُلْتُمْ سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu, na agano lake alilofungamana nanyi, mliposema: Tumesikia na tumetii. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua sana yaliyo ndani ya vifua.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu, na ahadi yake aliyo fungamana nanyi mlipo sema: Tumesikia na tumet'ii. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi sana wa yaliyomo vifuani.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70