يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَتَّخِذُوا۟ ٱلْيَهُودَ وَٱلنَّصَٰرَىٰٓ أَوْلِيَآءَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَآءُ بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُۥ مِنْهُمْ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلظَّٰلِمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki wandani. Wao kwa wao ni marafiki wandani. Na mwenye kuwafanya marafiki wandani miongoni mwenu, basi huyo hakika ni miongoni mwao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu madhalimu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniEnyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.