يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدْ جَآءَكُمُ ٱلرَّسُولُ بِٱلْحَقِّ مِن رَّبِّكُمْ فَـَٔامِنُوا۟ خَيْرًا لَّكُمْ وَإِن تَكْفُرُوا۟ فَإِنَّ لِلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi Watu! Hakika, amekwishawajia Mtume huyu kwa haki kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi aminini, ndiyo heri kwenu. Na mkikufuru, basi hakika ni vya Mwenyezi Mungu vilivyo katika mbingu na ardhi. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hekima.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniEnyi Watu! Amekwisha kujieni Mtume huyu na haki itokayo kwa Mola wenu Mlezi. Basi aminini, ndiyo kheri yenu. Na mkikakanusha basi hakika viliomo mbinguni na duniani ni vya Mwenyezi Mungu tu. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima.