وَٱلَّذَانِ يَأْتِيَٰنِهَا مِنكُمْ فَـَٔاذُوهُمَا فَإِن تَابَا وَأَصْلَحَا فَأَعْرِضُوا۟ عَنْهُمَآ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ تَوَّابًا رَّحِيمًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wawili kati yenu wafanyao hayo miongoni mwenu, waudhini. Na wakitubia wakatengenea, basi waacheni. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kupokea toba, Mwenye kurehemu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa wawili kati yenu wafanyao hayo waadhibuni. Na wakitubia wakatengenea basi waacheni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kupokea toba, Mwenye kurehemu.