وَمَن يُهَاجِرْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ يَجِدْ فِى ٱلْأَرْضِ مُرَٰغَمًا كَثِيرًا وَسَعَةً وَمَن يَخْرُجْ مِنۢ بَيْتِهِۦ مُهَاجِرًا إِلَى ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ ثُمَّ يُدْرِكْهُ ٱلْمَوْتُ فَقَدْ وَقَعَ أَجْرُهُۥ عَلَى ٱللَّهِ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mwenye kuhama katika Njia ya Mwenyezi Mungu, atapata pengi duniani pa kukimbilia, na atapata wasaa. Na mwenye kutoka katika nyumba yake akihamia kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kisha yakamfika mauti, basi hakika umekwishawajibika ujira wake kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa mwenye kuhama katika Njia ya Mwenyezi Mungu atapata pengi duniani pa kukimbilia, na atapata wasaa. Na anaye toka nyumbani kwake kuhama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kisha yakamfika mauti njiani basi umethibiti ujira wake kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu.