بَلَىٰٓ إِن تَصْبِرُوا۟ وَتَتَّقُوا۟ وَيَأْتُوكُم مِّن فَوْرِهِمْ هَٰذَا يُمْدِدْكُمْ رَبُّكُم بِخَمْسَةِ ءَالَٰفٍ مِّنَ ٱلْمَلَٰٓئِكَةِ مُسَوِّمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwani! Ikiwa mtavumilia na mkamcha Mungu, na hata maadui wakiwajia mara hii, basi hapo Mola wenu Mlezi atakusaidieni kwa Malaika elfu tano wenye alama maalumu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniKwani! Ikiwa mtavumilia na mkamchamngu na hata maadui wakikutokeeni kwa ghafla, basi hapo Mola wenu Mlezi atakusaidieni kwa Malaika elfu tano wanao shambulia kwa nguvu.