يَوْمَ تَبْيَضُّ وُجُوهٌ وَتَسْوَدُّ وُجُوهٌ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ٱسْوَدَّتْ وُجُوهُهُمْ أَكَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَٰنِكُمْ فَذُوقُوا۟ ٱلْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSiku ambapo nyuso zitakuwa nyeupe, na nyuso nyingine zikawa nyeusi. Basi, ama wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeusi (wataambiwa): Je, mlikufuru baada ya kuamini kwenu? Basi ionjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkikufuru.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniSiku ambayo nyuso zitanawiri na nyuso zitasawijika (kuwa nyeusi). Ama hao ambao nyuso zao zitasawijika wataambiwa: Je! Mlikufuru baada ya kuamini kwenu? Basi onjeni adhabu kwa vile mlivyo kuwa mnakufuru.