قَالَ هَلْ ءَامَنُكُمْ عَلَيْهِ إِلَّا كَمَآ أَمِنتُكُمْ عَلَىٰٓ أَخِيهِ مِن قَبْلُ فَٱللَّهُ خَيْرٌ حَٰفِظًا وَهُوَ أَرْحَمُ ٱلرَّٰحِمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Je, niwaamini juu yake isipokuwa kama nilivyowaamini kwa kakaye zamani? Lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mbora zaidi wa kulinda, naye ndiye Mbora zaidi wa wanaorehemu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniJe, nikuaminini kwa huyu ila kama nilivyo kuaminini kwa nduguye zamani? Lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mbora wa kulinda, naye ndiye Mbora wa kurehemu kuliko wenye kurehemu wote.