caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Hud, Aya 84

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 52 · 11:84

وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا قَالَ يَٰقَوْمِ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَٰهٍ غَيْرُهُۥ وَلَا تَنقُصُوا۟ ٱلْمِكْيَالَ وَٱلْمِيزَانَ إِنِّىٓ أَرَىٰكُم بِخَيْرٍ وَإِنِّىٓ أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ مُّحِيطٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa watu wa Madyana tuliwatumia ndugu yao Shu'aib. Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu yoyote isipokuwa Yeye, wala msipunguze vipimo na mizani. Mimi ninawaona mko katika hali njema, nami ninawahofia adhabu ya siku kubwa hiyo itakayowazingira.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa kwa watu wa Madyana tuliwatumia ndugu yao Shua'ib. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye, wala msipunguze vipimo na mizani. Mimi nakuoneni mmo katika hali njema, nami nakukhofieni adhabu ya Siku kubwa hiyo itakayo kuzungukeni.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70