caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Hud, Aya 31

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 52 · 11:31

وَلَآ أَقُولُ لَكُمْ عِندِى خَزَآئِنُ ٱللَّهِ وَلَآ أَعْلَمُ ٱلْغَيْبَ وَلَآ أَقُولُ إِنِّى مَلَكٌ وَلَآ أَقُولُ لِلَّذِينَ تَزْدَرِىٓ أَعْيُنُكُمْ لَن يُؤْتِيَهُمُ ٱللَّهُ خَيْرًا ٱللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا فِىٓ أَنفُسِهِمْ إِنِّىٓ إِذًا لَّمِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala siwaambii kuwa nina hazina za Mwenyezi Mungu, wala kuwa mimi ninajua mambo ya ghaibu, wala sisemi: Mimi ni Malaika. Wala sisemi kuhusu wale ambao yanawadharau macho yenu kuwa Mwenyezi Mungu hatawapa heri. Mwenyezi Mungu ndiye anayajua zaidi yaliyo katika nafsi zao. Hapo bila ya shaka nitakuwa miongoni mwa madhalimu."
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWala sikwambiini kuwa nina khazina za Mwenyezi Mungu; wala kuwa mimi najua mambo ya ghaibu; wala sisemi: Mimi ni Malaika. Wala siwasemi wale ambao yanawadharau macho yenu kuwa Mwenyezi Mungu hatawapa kheri - Mwenyezi Mungu anajua yaliomo katika nafsi zao - hapo bila ya shaka ninge kuwa miongoni mwa wenye kudhulumu.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70