وَمَا لَكُمْ لَا تُقَٰتِلُونَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱلْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ ٱلرِّجَالِ وَٱلنِّسَآءِ وَٱلْوِلْدَٰنِ ٱلَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَآ أَخْرِجْنَا مِنْ هَٰذِهِ ٱلْقَرْيَةِ ٱلظَّالِمِ أَهْلُهَا وَٱجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَٱجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mna nini hampigani katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na ya wale wanaoonewa miongoni mwa wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: 'Mola wetu Mlezi! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu, na tufanyie mlinzi kutoka kwako, na tufanyie wa kutunusuru kutoka kwako.'
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako.