إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَٱلَّذِينَ هَاجَرُوا۟ وَجَٰهَدُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ أُو۟لَٰٓئِكَ يَرْجُونَ رَحْمَتَ ٱللَّهِ وَٱللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika, wale walioamini, na wale waliohama na wakafanya juhudi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, hao ndio wanaotarajia rehema za Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniHakika wale walio amini na wale walio hama na wakapigania Njia ya Mwenyezi Mungu, hao ndio wanao taraji rehema za Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu.