وَمَآ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِىٓ إِلَيْهِم مِّنْ أَهْلِ ٱلْقُرَىٰٓ أَفَلَمْ يَسِيرُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ فَيَنظُرُوا۟ كَيْفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَدَارُ ٱلْـَٔاخِرَةِ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ ٱتَّقَوْا۟ أَفَلَا تَعْقِلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hatukuwatuma Mitume kabla yako isipokuwa wanaume tuliowafunulia ufunuo (wahyi) miongoni mwa watu wa mijini. Je, hawakutembea katika ardhi wakaona jinsi ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Na hakika nyumba ya Akhera ndiyo bora kwa wamchao Mungu. Basi hamtumii akili?
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa hatukuwatuma Mitume kabla yako isipo kuwa wanaume tulio wafunulia wahyi miongoni mwa watu wa mijini. Je! Hawatembei katika ardhi wakaona jinsi ulivyo kuwa mwisho wa walio kuwa kabla yao? Na hakika nyumba ya Akhera ni bora kwa wamchao Mungu. Basi hamfahamu?.